Kingoni

Kingoni ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania na Msumbiji inayozungumzwa na Wangoni. Kimetokana na lugha ya Kizulu Wangoni walipohama Afrika ya Kusini wakati wa Shaka Zulu. Mwaka wa 1887 idadi ya wasemaji wa Kingoni nchini Tanzania imehesabiwa kuwa watu 170,000. Pia kuna wasemaji 53,000 nchini Msumbiji. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kingoni iko katika kundi la N10.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search